Uzazi wa mpango | kwanini ni muhimu

Uzazi wa mpango | kwanini ni muhimu

Bado watu wengi hawajafahamu kwamba uzazi wa mpango ni njia muhimu sana katika kuinua hali ya afya ya mama na mtoto. Uzazi wa mara nyingi au wa karibu au wa wanawake wenye umri mkubwa au wa wasichana wenye umri mdogo husababisha karibu theluthi moya ya vifo vya watoto wachanga duniani
Hivyo mambo muhimu manne yatasaidia katika kuzuia vifo vya mamilioni ya watoto pamoja na mamia ya maelfu ya wanawake kila mwaka.

  1. Kupata mimba kabla ya kufikia umri wa miaka 18 au baada ya umri wa miaka 35 huongeza hatari kwa afya ya mama na mtoto
  2. Uwezekano wa vifo vya watoto wadogo huweza kuongezeka kwa karibu asilimia 50 iwapo kipindi kati ya uzazi wa motto mmoja na anayefuata ni chini ya miaka miwili
  3. Uzazi wa Zaidi ya watoto wane huongeza matatizo ya uja-uzito na uzazi
  4.  Kuna njia nyingi salama na zinazokubalika ili kuzuia mwanamke asipate mimba. Huduma za uzazi wa mpango zitaweza kuwapa mume na mke maarifa na uwezo wa kupanga wakati wa kuanza kupata watoto, kipindi kati ya uzazi wa motto mmoja na mwingine na lini kuacha kuzaa

Wanawake Zaidi ya nusu milioni hufa kila mwaka kutokana na matatizo yanayohusiana na mimba na uzazi na kuwaacha watoto zaidi ya milioni moja wakiwa hawana mama. Vifo vingi kati ya hivi vingeweza kuzuilika kwa kutumia na kuzingatia maarifa ya kisasa kuhusu kupanga mimba
Wasichana wote wapewe fursa ya kukomaa na kuwa watu wazima kabla ya kuwa wazazi. Katika jamii ambazo wasichana huolewa wakiwa na umri mdogo, mume na mke washauriwe kuchelewesha uzazi wa kwanza hadi msichana atakapotimiza umri wa miaka 18.

Kwasababu za kiafya pekee, msichana anashauriwa asipate mimba kabla ya kutimiza umri wa miaka 18. Kimaumbile msichana hajawa tayari kuanza kuzaa hadi anapotimiza miaka 18 au Zaidi. Watoto wanaozaliwa na wanawake ambao hawajafikisha umri huo, maranyingi huzaliwa wakiwa na uzito mdogo kuliko unaotakiwa na huzaliwa kabla ya wakati. Uzazi wa wanawake kama hao, mara nyingi huwa wa matatizo. Uwezekano wa watoto wanaozaliwa na wanawake hao kufa katika mwaka wao wa kwanza ni mkubwa. Pia afya ya mama hao huwa hatarini.

Baada ya umri wa miaka 35 matatizo ya kiafya wakati wa uzazi na uja uzito huanza kuongezeka tena. Kwa mwanamke ambaye ana umri wa Zaidi ya miaka 35 na amekuwa mja mzito mara nne au Zaidi, mimba inayofuata itahatarisha Zaidi afya yake naya mtoto anayetarajiwa kuzaliwa.

Leave a Reply

%d bloggers like this: